Tuesday, November 11, 2008

About me


NI Mimi Mawazo Lusonzo, ni mwandishi wa habari mwandamizi katika kampuni ya LadyBand inayochapisha magazeti ya Changamoto na The Football.Magazeti yote haya yanachapishwa kwa lugha ya Kiswahili.
Gazeti la Changamoto, linaandika habari nyingi za uchunguzi, siasa, jamii, uchumi, michezo na burudani, huwa mitaani kila siku ya Jumanne.The Football, hili ni gazeti la michezo na burudani, ambalo linatoka kila jumamosi.
Ndani ya kampuni ya LadyBand inayochapa magazeti haya, mimi ninabeba jukumu la mhariri wa michezo wa magazeti yote mawili.
Ni mzaliwa wa mwaka 1964 katika mji mdogo wa Mkongo, uliopo wilayani Rufiji, mkoani Pwani.Kabila langu ni Mkutu, na asili yangu ni mkoa wa Morogoro, katika kitongoji kongwe cha Maji Moto, Kisaki.
Nimeingia katika taaluma hii ya uandishi wa habari mwaka 1993 na kuandikia magazeti mbalimbali yakiwemo, Wasaa, Majira,Maisha, Dar Leo, Mkombozi,Watu, Mwangaza,Ngurumo za Simba na sasa Changamoto na The Football.
Ni mwandishi wa makala, habari za uchunguzi, siasa, burudani, ambapo kwa sasa nimejikita katika masuala ya michezo na burudani.


Nilichojifunza katika kozi hii ni kuwa:-

1. Matumizi ya makubwa ya Internet inavyosaidia katika kupata taarifa nyingi kwa ajili ya kupata taarifa za usafiri, hali ya hewa, masuala ya benki, usomaji wa vitabu duniani kote.
2. Nimejifunza upatikanaji rahisi wa habari mbalimbali kupitia Internet.
3.Kwa misingi hii, na kwa lugha nyepesi ni sawa na kusema kuwa, Internet ni kila kitu, na imeifanya dunia kuwa kama kijiji.

No comments: