Friday, November 14, 2008

Maoni yangu kupitia kozi hii

NILIKUWA mmoja wa washiriki wa Semina iliyoandaliwa na MISA Tan, iliyojumuisha Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya hapa nchini.
Semina hiyo ilihususha pia na waandishi wa habari waandamizi, pamoja na wale wanaoendelea kujifunza fani hiyo.

Semina hiyo iliyoanza Novemba 10 hadi 14 mwaka huu, pamoja na mambo mengi tuliweza kujifunza teknolojia ya kompyuta na vipengele vyake, kikubwa zaidi tulijifunza matumizi ya Internet na matumizi yake katika fani ya uandishi wa habari kote duniani.

Katika mada hiyo, tumejifunza kuwa,matumizi ya Internet ni makubwa, ama kwa lugha nyingine ni kwamba, Internet inaweza kutumika kama nyenzo kubwa ya upatikanaji wa habari katika vyombo vingi vya habari.

Hii ni kwa sababu, kwa kutimia Internet mwandishi ama chombo cha habari husika kinaweza kupata taarifa kutoka kila kona ya dunia, na ndipo unapokuja msemo usemao kuwa, kwa kutumia kompyuta ni dunia ni kama kijiji, ambapo unaweza ukapata taarifa muhimu kupitia mitandao mikubwa ya habari duniani.

Wito wangu, ambalo ni pendekezo langu kwa MISA Tan kupitia kozi hii ni kwamba, pamoja na kushukuru kwa kina kufanyika kwa kozi hii na mimi kuwa mmoja wa mshiriki, ningependekeza kuwa, wakati umefika sasa kwa taasisi yetu hii kuandaa kozi nyingi kama hizi, na kuwashirikisha waandishi wengi wa habari kutoka katika vyombo vingi, na hii itasaidia kuwapa uwezo wa kujifunza jinsi ya kutumia teknolojia za kisasa kupata habari na taarifa muhimu kutoka kokote duniani.
Kufanyika kwa kozi nyingi kama hizi zitasaidia waandishi na taaluma kwa ujumla kufanya kazi zao kirahisi na kwenda na wakari kana walivyo waandishi na vyombo vya habari vya nchi zilizoendelea.

No comments: